





Orodha kamili ya vipimo vya ultrasound
| Kipimo | Kinatumika kwa nini |
|---|---|
| Ultrasound ya Ujauzito (Obstetric) | Huchunguza ujauzito, hufuatilia ukuaji wa mtoto tumboni, mkao wake na afya yake. |
| Ultrasound ya Figo na Kibofu (KUB) | Huchunguza figo, mirija ya mkojo na kibofu kuangalia mawe, kuziba na kasoro nyingine. |
| Ultrasound ya Nyonga (Pelvic) | Huchunguza mfuko wa uzazi na ovari kutambua fibroids na uvimbe kwenye nyonga. |
| Ultrasound ya Tumbo (Abdominal) | Huchunguza ini, kifuko cha nyongo, kongosho, wengu na figo. |
| Ultrasound ya Mishipa ya Damu (Doppler) | Hupima mtiririko wa damu kugundua mishipa iliyobana, iliyoziba au mzunguko usio wa kawaida. |
| Ultrasound ya Shingo | Huchunguza tezi ya koo (thyroid), tezi za limfu na tishu laini. |
| Ultrasound ya Dharura (FAST) | Uchunguzi wa haraka wa dharura kuangalia damu inayovuja ndani ya tumbo au kuzunguka moyo. |
| Ultrasound ya Matiti | Huchunguza uvimbe na vifuko vya maji kwenye matiti. |
| Ultrasound ya Tishu Laini | Huchunguza uvimbe ulio chini ya ngozi, maji yaliyokusanyika na majipu. |
| Ultrasound ya Tumbo na Nyonga | Huchunguza viungo vya tumbo na nyonga kuangalia kasoro. |
| Ultrasound ya Korodani | Hugundua kasoro na maambukizi kama vile mshipa (hydrocele). |
Gundua zaidi
Kurasa zinazohusiana
Uko tayari kuweka miadi ya picha za uchunguzi?
Tuandikie kwa WhatsApp unachohitaji nasi tutakuthibitishia miadi yako.
